Kutembelea kliniki ya meno kwa mara ya kwanza

Kutembelea kliniki ya meno kwa mara ya kwanza kunaweza kuwa jambo la kusisimua na la kustaajabisha kidogo, tunapoangalia meno kwa mara ya kwanza.
No items found.

Maandalizi

Mtoto anahitaji kujiandalia shughuli itakayofanywa katika kliniki ya uchunguzi wa meno. Kabla ya kutembelea kliniki, inashauriwa umfanyishe mtoto mazoezi ya kufungua kinywa wazi mbele ya kioo unapohesabu meno. Mwambie kuhusu kiti, taa na kioo kidogo ambacho hutumiwa kuchunguza meno yake. Inaweza pia kuwa muhimu kutumia kifaa cha kukagua meno ili kuchunguza meno yake kidogo katika ziara ya kwanza.

Usalama

Ziara hii ni ya kuweka msingi wa uhusiano wa kuaminiana ambao unatarajiwa kudumu maisha yote, na madaktari wa meno watahakikisha kuwa uchunguzi wa meno utakuwa shughuli ambayo kila mtu ataipenda.

Mtoto atakuwa mhudumiwa mkuu, na wazazi watagundua kuwa mtaalamu wa afya ya meno atamwongelesha mtoto moja kwa moja. Atachukua muda mrefu inavyohitajika kuzungumza naye kumpa mtoto ujasiri anaohitaji.

Iwapo mtu atakayeandamana na mtoto hataogopa kumtembelea mtaalam/daktari wa meno, pia atasaidia mtoto ujasiri kuwa shughuli hii ni salama. Wasiliana na kliniki ya meno kabla ya ziara na uwajulishe wahudumu ikiwa mtoto anaogopa sana. Pamoja mtaweza kupata mbinu inayomfaa mtoto wako.

Afya ya meno ya mtoto

Utapokea maelezo na mwongozo kuhusu hatua zinazohitajika ili kudumisha afya bora ya meno. Ni wajibu wa huduma ya meno kwa umma kukushauri kuhusu jinsi ya kuifanya vyema kazi hii.

Uliza kama kuna chochote ambacho huelewi - masuala yoyote makubwa na madogo kuhusu afya ya meno ya mtoto wako. Tujulishe kuhusu magonjwa, dawa au matatizo ya lishe. Mambo haya yanaweza kuathiri afya ya meno.

No items found.