Afya njema ya meno kuanzia jino la kwanza

Kutokea kwa jino la mtoto wa kwanza kunaashiria hatua mpya katika ukuaji wa mtoto wako. Ni muhimu kudumisha mitindo bora ya afya ya meno mapema.
No items found.

Kuota meno

Meno ya mbele katika taya ya chini kawaida huota kwanza. Kwa kawaida meno haya huota mtoto akiwa na umri wa miezi 6-8. Kisha, meno ya mbele katika taya ya juu huota, yakifuatiwa na chego za mbele, chonge na hatimaye chego za nyuma. Mtoto wako atakuwa na meno yake yote ya utotoni, 10 katika taya ya juu na 10 katika taya ya chini, anapokisha umri wa miaka 3.

Ni kawaida kwa watoto kuwashwa ufizi wakati meno yanaota, na kawaida hupenda kutafuna vitu. Wape kifaa cha kutafunia kinachofaa cha mpira mgumu au plastiki, kisicho na makali. Baadhi ya watoto hupatwa na wasiwasi na wanaweza kupata usumbufu fulani, lakini kuota meno hakupaswi kusababisha homa ya juu na ya muda mrefu.

Kupiga mswaki

Watoto wanapaswa kuanza kupigwa mswaki punde tu jino la kwanza linapotokea kinywani. Tumia mswaki mdogo, laini na kiasi kisichoonekana cha dawa ya meno ya floridi. Huenda dawa ya meno ya watoto iwe na ladha ndogo. Ongeza kiasi cha dawa ya meno ya floridi itoshane na ukucha wa kidole cha mtoto wako katika umri wa mwaka mmoja, na hadi ukubwa wa mbegu ya kunde akiwa na umri wa miaka 3. Akiwa umri wa miaka 5-6, kiasi hiki kinaweza kuongezwa. Wizara ya Afya inapendekeza kwamba watoto wanapaswa kusaidiwa kupiga meno mswaki hadi waweze kujipiga mswaki vizuri, kawaida karibu umri wa miaka 10.

Dawa ya meno inahitaji kupewa muda ili ifanye kazi, hivyo epuka kula chakula na kunywa vinywaji hadi saa moja baada ya kupiga mswaki. Ikiwa hutumii dawa ya meno ya floridi, au ikiwa mtoto wako anahitaji floridi zaidi, vidonge vya floridi vinaweza kuwa chaguo nzuri. Fuata ushauri unaopewa katika kliniki ya afya ya umma/meno.

Matundu

Sukari husababisha matundu kwenye meno. Mtoto anapokula au kunywa kitu chenye sukari, bakteria zilizo kinywani mwake zitazalisha asidi ambayo inaweza kuyeyusha gamba la meno na kusababisha matundu. Haya yote hutegemea ni mara ngapi mtoto anakula au kunywa kitu kilicho na sukari. Mate huondoa makali ya asidi inayozalishwa baada ya kila mlo. Kwa hiyo, ni muhimu kuu asile au kunywa chochote kilicho na sukari katikati ya vipindi vya mlo, na hasa usiku wakati kiasi kinachozalishwa ni kidogo.

Kunyonyesha

Maziwa ya mama huwa na sukari ya maziwa ambayo kwa kiasi fulani yanaweza kugeuzwa kuwa asidi. Kiasi cha mate yanayolishawa hupungua usiku, jambo ambalo huongeza hatari ya kuoza meno. Mzazi anapaswa kupunguza kumnyonyesha au kumpa maziwa ya chupa mara nyingi baada ya mtoto kufikisha umri wa mwaka mmoja.

Mpangilio wa meno

Kunyonya kidole gumba au kifaa cha kutuliza huwafariji watoto wadogo. Tabia za kunyonya kidole zinaweza kusababisha mpangilio wa meno kuharibika, lakini kawaida meno yatapangika yenyewe ikiwa mtoto ataacha kunyonya kidole gumba/kifaa cha kutuliza kabla ya kuanza kung’oka meno ya utotoni.

Ajali

Kuanguka au kugongwa kinywani kunaweza kuharibu jino moja au mengi. Kwa hivyo ni muhimu kuwasiliana na kliniki ya meno iliyo karibu ili uripoti kuhusu ajali na upate huduma sahihi ya ufuatiliaji.

Mapngo wa huduma za afya ya meno kwa umma

Huduma ya meno kwa umma inawajibikia utunzaji wa meno wa watoto na vijana baleghe wa kutoka umri wa miaka 0 hadi 18. Watoto hawa hupelekwa kufanyiwa uchunguzi wao wa kwanza wa afya ya meno katika kliniki ya meno wanapofikisha umri wa miaka 3. Kabla ya hapo, kliniki ya afya ya umma (helsestasjonen) itafuatilia tabia na afya ya meno na tabia. Watapewa rufaa ya huduma ya meno kwa umma na muuguzi/daktari wa afya ya umma, ikiwa wanahitaji kufanyiwa tathmini ya meno kabla ya uchunguzi wa kawaida wakifikisha miaka 3.

Wasiliana na kliniki ya meno ya umma iliyo karibu ikiwa unahitaji maelezo zaidi.

No items found.